Friday, 30 March 2018

Wabunge Chadema waandamana EU
Wabunge Chadema wakiwa ofisi za EU

WABUNGE na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), jana mchana (Machi 29, 2018) waliandamana kwenda ofisi za Umoja wa Ulaya (EU).

Wabunge hao wamekwenda katika ofisi hizo kulalamikia kile wanachofanyiwa viongozi sita wa chama hicho akiwamo mwenyekiti wa wake, Freeman Mbowe waliopo mahabusu.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema, “Tuko EU (Umoja wa Ulaya). Tupo wabunge wote tumeandamana kuja hapa kuleta kilio chetu.”
 
Miongoni mwa Viongozi waliofika katika ubalozi huo ni Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, Meya wa Ubungo Boniface Jacob ambapo wametahadhalisha usalama wa viongozi hao pamoja wafuasi wa chama hicho.

No comments:

Post a Comment