Saturday, 24 March 2018

Wajua kitunguu swaumu ni moja ya dawa za vidonda kinywa na koo?

Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akionesha vitunguu swaumu ambavyo ni moja ya tiba za tatizo la kinywa na koo.


TATIZO la vidonda vya kinywa na koo linapompata mwanadamu vinampa wakati mgumu kwani pamoja na mambo mengine humfanya ashindwe kula na kumwia vigumu kuzungumza.

Ingawa vidonda humfanya mtu ajisikie vibaya, huwa vinapona vyenyewe ndani ya wiki moja au mbili.

Vidonda vya kinywa huweza kutokea kwenye mashavu, midomo , ulimi, kingo na kuta za meno pia huweza kusambaa hadi kwenye koromeo ikiwa havitatibiwa kwa wakati.

Tiba ya maji ya moto yaliyoongezwa chumvi yanaposukutuliwa mdomoni na kuachwa yasogee karibu na koo kutwa mara tatu muda mfupi kabla ya mlo husaidia kuponya haraka vidonda.

Pia tumia vipande vidogo vya tangawizi vitie mdomoni na kutafuna taratibu huku ukimeza maji yake vikiisha kula vingine, vina saidia kuponya vidonda vya mdomo na kooni.

Chemsha robo kilo ya majani ya mzeituni na maji yake sukutua mdomoni kutwa mara mbili.

Osha vizuri jani la aloevera kata vipande vidogo tia mdomoni na tafuna taratibu huku ukifyonza maji yake, vikiisha tia vingine.

Menya kitunguu swaumu kimoja, tia kinywani kwa muda ukitafuta polepole na kumeza maji yatokanayo.

Ukikumbwa na tatizo hilo ni vema uje katika ofisi zetu kupata maelezo stahiki ya namna ya kutumia tiba tajwa kutoka kwa mtaalam wetu.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment