Monday, 5 March 2018

Wajua mtunguja unasaidia kukabili mkanda wa jeshi?

Mtunguja 


MKANDA wa jeshi ni ugonjwa unaotoa malenge lenge mfano wa tetekuwanga.

Badala ya kusambaza mwili mzima, ugonjwa huo hushambulia sehemu maalum za mwili kama uso, mgongo, sehemu ya kifua, chini ya kwapa, shingoni na kwenye paja.

Mkanda wa jeshi unasababishwa na virusi na ni ugonjwa ambao hauna tiba maalumu, dawa zinazotumika kutibu mkanda wa jeshi kwa ajili ya kupunguza maumivu, kuzuia kuahirika kwa nevu na kukausha malengelenge kwa muda mfupi iwezekanavyo.

Zipo dawa asili nyingi ambazo zinasaidia kukabiliana na tatizo hilo ambazo ni pamoja na udongo mwekundu, mtunguja au mtaa pamoja na mbono.

Udongo mwekundu

Chukua udongo mwekundu unaotumika kutengeneza matofali ya kuchoma, kanda kwa muda wa nusu saa ili kuua vijidudu vinavyoweza kuwa ndani yake.

Chekecha ili kupata unga laini unaoweza kunyunyizia sehemu iliyoathirika kwa mkanda wa jeshi. Fanya hivyo asubuhi na jioni hadi utakapo pona

Mtunguja au mtaa

Ponda mtunguja (sehemu zote za mmea zinafaa) uwe katika uji laini, paka sehemu zilizoathirika wakati wa asubuhi na jioni. Endelea na tiba hiyo hadi utakapo pona.

Mbono

Chukua utomvu wa mbono, paka sehemu zote zenye malenge lenge. Fanya hivyo asubuhi na jioni hadi ugonjwa utakapo pona.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Yeyote anayesumbuliwa na tatizo la kiafya na ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Mandai kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

No comments:

Post a Comment