Tuesday, 27 March 2018

Wajumbe PAC watembelea Mradi wa Rocky City Mall


Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC)  wakiwasili katika Jengo la Rocky City Mall lililopo Jijini Mwanza kwa ajilil ya kukagua mradi huo uliotekelezwa kwa ubia kati ya halmashauri ya jiji la Mwanza na Mfuko wa Pensheni wa LAPF. Mbele ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Naghenjwa Kaboyoka na Mkurugenzi Mkuu wa LAPF, Eliudi Sanga.


Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC),  wakiwa katika kikao cha pamoja na uongozi wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF na halmashauri ya jiji la Mwanza kujadili utekelezaji wa mradi wa jengo la  Rocky City Mall unaotekelezwa kwa ubia kati ya halmashauri ya jiji hilo na LAPF.


Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), wakioneshwa baadhi ya maeneo ndani ya jengo la Rocky City Mall. Pichani wakiangalia chumba ambacho kinadhibiti hali ya usalama katika maeneo ya jengo hilo (control room).

No comments:

Post a Comment