Friday, 9 March 2018

Wanne wadaiwa kufa ajali ya Mbarali


BASI la kampuni ya Super Rojas lenye namba za usajili T 170 DKS limegongana na lori na kusababisha vifo vya watu wanne na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa.

Ajali hiyo ilitokea jana eneo la Igawa, Mbarali mkoani Mbeya, ambapo mashuhuda wanasema chanzo ni dereva wa basi ambaye alikuwa akijaribu kukwepa tawi la mti lililokuwa limeegeshwa barabarani kuonesha ishara ya kuwepo gari bovu mbele.

Basi hilo lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Njombe, liligongana na lori hilo lenye namba za usajili T 838 DRE aina ya Scania lililokuwa limebeba kontena. Ajali hiyo imetokea katika barabara inayounganisha mikoa ya Mbeya na Iringa. 

No comments:

Post a Comment