ZIPO
tiba nyingi wanazitumia matabibu kuwaganga watu (mtu) wanapotokwa damu baada
kujeruhiwa.
Miongoni
mwazo ni pamoja na utando wa buibui, maji baridi na jivu, ugoro na tumbaku,
chokaa, mkaa, bizari na chokaa, bizari na chumvi, embe, muarobaini na mpungate.
Utando
wa buibui
Baada
ya kujikata au kuumia kama kidonda siyo kikubwa sana, kioshe kwa maji ya chumvi
halafu weka utando wa buibui. Utando huo una dawa inayoitwa akinidini ambayo
inasaidia sana kugandisha damu.
Maji
baridi na jivu
Kitambaa
safi kiweke ndani ya maji baridi kisha kitoe harafu kanda katika jeraha, kama damu
inaendelea kutoka, chukua jivu la pamba au kitambaa hariri weka kwenye jeraha.
Jivu la kuni au mkaa pia bandike katika kidonda linasaidia pia.
Ugoro
na tumbaku
Baada
ya kuumia, safisha kidonda, nyunyizia ugoro au tumbaku, nikotini iliyomo kwenye
tumbaku huifinya mishipa isitoe damu.
Chokaa
Weka
chokaa katika kidonda kuzuia kuvuja damu, baada ya hapo kunywa glasi moja au
mbili za maji baridi.
Mkaa
Osha
kidonda kwa maji yenye chumvi, nyunyizia unga wa mkaa katika sehemu ya jeraha,
kunywa glasi moja au mbili za maji baridi
Bizari
na chokaa
Changanya
bizari iliyopondwa na unga wa chokaa, weka sehemu yote ya jeraha damu itaacha
kutoka.
Bizari
na chumvi
Changanya
bizari na chumvi, weka kwenye jeraha itazuia damu kuendelea kutoka.
Embe
Mbegu
ya embe, majani ya mwembe au gome lake, choma mojawapo ili kupata majivu, weka
kwenye jeraha linalovuja damu, itakoma kutoka.
Muarobaini
Ponda
majani ya muarobaini bandika kwenye jeraha.
Mpungate
Ikiwa
umekosa maji safi ya kusafishia kidonda safisha kidonda kwa kutumia utomvu wa mpungate.
Kata
kipande cha mpungate, funga kwenye jeraha, baada ya saa tatu ondoa safisha
kidonda kwa sabuni na maji yaliyochemshwa.
Mchanganuo
huu umeletwa kwako na mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.
Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya
karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na
Mtaalam Mandai kwa simu
+255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri
au virutubisho vyetu.
No comments:
Post a Comment