Saturday, 17 March 2018

Waziri mkuu wanafunzi chuo kikuu wafundishwe mbinu za kujiaria baada ya kuhitimuWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) alipokutana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa William Anangisye, ofisini kwake Mjini Dodoma jana.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema ni vema mfumo wa ufundishaji   wanafunzi wa vyuo vikuu nchini ukaboreshwa ili wanapomaliza waweze kujiajiri.

“Kumekuwa na tatizo wasomi wetu wana mtazamo kwamba wanapomaliza masomo yao lazima waajiriwe. Upo umuhimu wa kubadili mtazamo huo kwa kuwapa mbinu zitakazowawezesha kujiajiri.”

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Ijumaa, Machi 16, 2018) alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye, ofisini kwake mjini Dodoma.

Amesema wanafunzi wanapomaliza wanatakiwa wawe na uwezo wa kubuni mbinu mbalimbali za kujiajiri ili kuondokana na mtazao wa kusubiri ajira za kuajiriwa maofisini.

Waziri Mkuu amesema wasomi hao wanaweza kuchukua kauli mbiu ya Rais Dk. John Magufuli ya uchumi wa viwanda kwa kuanzisha kilimo cha mazao mbalimbali yatakayotoa malighafi za viwandani.

Pia Waziri Mkuu amesema wasomi hao wanaweza kujikita katika shughuli za uchimbaji wa madini au usindikaji wa mazao mbalimbali, hivyo tayari watakuwa wamejiajiri kwa sababu ajira si za ofisini pekee.

Aidha, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumpongeza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyestaafu Profesa Rwekaza Mukandara kwa kazi nzuri aliyoifanya kipindi cha uongozi wake.

Kwa upande wake, Profesa Anangisye amesema mzigo aliopewa wa kuiongoza taasisi hiyo si mwepesi, hivyo ameahidi kufanya kazi kwa bidii na hatokwenda kinyume na matarajio ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Kiongozi huyo amesema katika kuhakikisha wanaboresha masomo chuoni hapo wameanzisha shule ya kilimo na uvuvi, hivyo watakuwa na mashamba ya mfano kwa ajili ya mazao mbalimbali.
Shar

No comments:

Post a Comment