Thursday, 22 March 2018

Waziri wa ulinzi wa Israel Avigdor Liberman  akimpa zawadi mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel alipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jana huku waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy Mwalimu akishuhudia. Tangu mwaka 2015 JKCI kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel wanafanya kambi maalum za matibabu ya moyo  kwa watoto.Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto Ummy Mwalimu na Waziri wa ulinzi wa Israel, Avigdor Liberman  wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto na wazazi wao ambao wamefanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel.  Liberman alitembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jana kwa ajili ya kuona ushirikiano ulipo kati ya JKCI na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel ambao kwa kushirikiana wanafanya kambi maalum za matibabu ya moyo kwa watoto ambapo watoto wanaokutwa na matatizo yanayohitaji matibabu ya hali ya juu wanatibiwa nchini humo bila malipo.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto Ummy Mwalimu akimpa zawadi ya kitenge Waziri wa Ulinzi wa Israel, Avigdor Liberman alipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jana kwa ajili ya kuona ushirikiano ulipo kati ya JKCI na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH). 


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy Mwalimu na Waziri wa Ulinzi wa Israel, Avigdor Liberman wakiwa katika picha ya pamoja na madaktari pamoja na wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambao walisoma nchini Israel kwa udhamini wa Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini humo.


No comments:

Post a Comment