Thursday, 22 March 2018

Ziara ya Waziri wa Ulinzi wa Israel, Avigdor Lieberman Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais Dk. John Magufuli akisalimiana na Waziri wa Ulinzi wa Israel, Avigdor Lieberman mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo.Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Waziri wa Ulinzi wa Israel, Avigdor Lieberman wa kwanza (kushoto kwake) Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa Dk. Hussein Mwinyi wa nne kutoka (kulia) Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Florence Turuka wa kwanza kushoto aliyesimama mstari wa nyuma pamoja na Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama na makamanda mbalimbali kutoka makao makuu ya jeshi.Rais Dk. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Waziri wa Ulinzi wa Israel, Avigdor Lieberman mara baada ya kikao chao Ikulu Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment