Friday, 16 March 2018

Zingatia moja ya tiba hizi unapokumbwa na kikohozi kisicho cha kawaida


Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akielezea namna kikohozi kisicho cha kawaida kinavyoweza kudhibitiwa.

KIKOHOZI  kinaweza kuenezwa na kichocheo ndani ya koo, mabadiliko ya hewa au majira au kuziba mifereji ya kupitisha hewa ndani ya mapafu.

Lengo la kukohoa ni kutoa chembechembe zisizohitajika katika njia ya kupitishia hewa. Kikohozi cha kawaida kinaweza kupona bila dawa ya aina yoyote.

Unaweza kutibu kikohozi kwa kutumia zabibu, asali, bizari, kitunguu swaumu, tofaa, karafuu, tangawizi, kitunguu, chumvi, msubili na limau.

Zabibu

Tumia juisi ya zabibu kwa sababu ina uwezo mkubwa wa kuhamasisha mapafu kutoa makohozi. Chukua glasi moja ya juisi ya zabibu, ongeza asali kijiko kimoja cha mezani kunywa kwa ajili ya kutibu kikohozi. Tumia juisi hii kwa muda wa siku tatu hadi wiki moja.

Asali

Tumia asali kijiko kimoja cha mezani mara tatu kwa siku kwa maana ya asubuhi, mchana na jioni kwa muda wa siku tatu hadi saba.

Bizari

Kijiko kimoja cha unga wa bizari, weka ndani ya sukari kisha kaanga kidogo, ongeza maziwa nusu glasi, endelea kupasha moto kwa dakika tatu. Ipua mchanganyiko huo kisha weka ndani ya kikombe, ongeza asali kijiko kimoja cha chai, kunywa. Tumia mara tatu kwa siku kwa muda wa siku tatu.

Kitunguu swaumu

Saga punje sita za kitunguu swaumu, changanya na nusu glasi ya maji moto kunywa asubuhi na jioni kwa muda wa siku tatu.

Tofaa (Aplles)

Tumia tofaa tamu robo kilo kwa siku kwa muda wawiki moja.

Karafuu na chumvi

Ponda karafuu tatu, changanya na asali kijiko kimoja cha mezani. Weka mchanganyiko huo katika sehemu mbili zinazolingana , ongeza chumvi kidogo, lamba taratibu asubuhi na jioni. Tiba hii ya siku tatu hadi saba.

Msubili

Jani la msubili kata kata vipande vya nusu futi, kunywa juisi ya kipande kimoja cha msubili iliyoongezwa chumvi. Tumia kutwa mara tatu kwa siku. Endelea na tiba hii kwa muda wa siku nne.

Limau

Limau nane zikate katikati kila moja, weka ndani ya lita mbili za maji, ongeza punje nane za kitunguu swaumu zilizopondwa, tangawizi moja na nusu na kitunguu maji vyote viwe vimepondwa, vichemshe kwa muda wa dakika tano, tumia nusu kikombe cha mchanganyiko huo mara tatu kwa muda wa siku tano.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Mandai kwa ushauri au kujipatia kirutubisho.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment