Saturday, 10 March 2018

Zingatia njia hizi kukabili tatizo la kukosa kumbukumbu


Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai

ILI kukabiliana na tatizo la kukosa kumbukumbu  zipo njia mbalimbali ukizitumia unaweza kuondokana nalo. Unaweza kula bamia, maua ya komamanga, mtindi, wali, rozimeri, tofaa, pilipili manga na methi.

Bamia

Tumia mara nyingi uwezavyo bamia isiyopikwa muda mrefu.

Maua ya komamanga

Maua chipukizi ya komamanga yakaushe katika kivuli. Saga unga utunze katika chupa safi yenye mfuniko. Tumia nusu kijiko cha chai cha unga huo katika maji ya uvuguvugu mara tatu kwa siku muda wa mwezi mmoja.

Mtindi/wali

Tindikali glutamiki iliyoko katika mchele, inaaminika kuhamasisha utendaji kazi mzuri ndani ya ubongo wa mwanadamu. Kula wali kwa mtindi kila jioni mara nne kwa wiki kwa muda wa miezi mitatu.

Rozimeri

Tengeneza kikombe kimoja cha chai  ya majani ya rozimeri (mabichi au makavu), ongeza asali kijiko kimoja cha mezani, koroga  kisha kunywa. Fanya hivyo asubuhi na jioni kwa muda wa miezi miwili hadi mitatu.

Tofaa

Kula tofaa moja kila asubuhi hadi utakapoondokana na tatizo hilo.

Pilipili manga

Nusu kijiko cha pilipili manga changanya na kingine cha chai cha asali, lamba kidogokidogo mara mbili kutwa, asubuhi na jioni.

Methi

Kila jioni kabla ya chakula cha usiku, kula saladi ya majani ya methi kiasi cha kujaa sahani ya chai, kwa ajili kuongeza uwezo wa kumbukumbu.
Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Mandai kwa ushauri au kujipatia kirutubisho.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment