Wednesday, 11 April 2018

36 wahukumiwa kifo Misri kwa kushambulia makanisa ya CopticRais wa Misri, Abdal Fattah Al- Sisi
MAHAKAMA ya kijeshi nchini Misri imewahukumu watu 36 adhabu ya kifo kwa kosa la kushambulia makanisa ya Coptic.
Watu 70 walifariki dunia kutokana na shambulio la bomu katika kanisa kuu la ki - Coptic mjini Cairo mwishoni mwa mwaka 2016, na makanisa ya Alexandria na Tanta siku kama hiyo mwezi Agosti mwaka uliofuata.
Tayari kundi la wanamgambo wa kiislamu wenye msimamo mkali wamekiri kuhusika na mashambulizi hayo matatu. Wameendelea kukiri kuwa kazi yao kubwa ilikuwa kuwashambulia wakristo wachache, pamoja na mamlaka ya kijeshi.
Misri inahitaji mahakama kupeleka kesi za namna hiyo kwa Mufti mkuu nchini humo kwa kuzingatia adhabu ya kifo kabla ya hukumu ya mwisho.

No comments:

Post a Comment