Monday, 9 April 2018

Adhabu ya kifo yashutumiwa Mali


Mlinzi wa amani nchini Mali, akilinda usalama
KIKUNDI cha kutetea haki za binaadamu nchini Mali kimelilaumu jeshi la nchi hiyo kutokana na kitendo cha kutekeleza adhabu ya kifo kwa wafungwa 14 katikati mwa jiji la Dioura.
Jeshi la nchi hiyo liliarifu kuwa wafungwa hao walikamatwa Alhamisi wiki iliyopita na kuuawa muda mfupi tu baadaye.
Ndugu wa marehemu, ambao wanatoka katika kundi la kabila la Fulani, wamesema ndugu zao hawakuwa na ushirikiano wa aina yoyote na makundi ya vijana wenye msimamo mkali.
Jamii hiyo ya kabila la Fulani imelalamika kuwa hii si mara ya kwanza kuhusishwa na makundi yenye msimamo mkali wa kidini.
Wiki hii, wanaharakati wa kundi la haki za binadamu la Amnesty International wamearifu kuwa wanaume sita walikutwa wamezikwa katika kaburi la halaiki mapema mwezi uliopita ambao walitiwa mikononi mwa jeshi siku tatu nyuma.
Chanzo BBC

No comments:

Post a Comment