Tuesday, 3 April 2018

Almas Jumaa: Mbunge mmoja yupo ICU


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma Taasisi ya Mifupa (Moi), Almas Jumaa wa kwanza kulia.

Mwandishi Wetu

MBUNGE Haji Ameir Haji (Makunduchi), yupo kwenye chumba maalumu za uangalizi (ICU), katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI).
Haji Ameir Haji na wenzake wanne walipata ajali Machi 29, mwaka huu mkoani Morogoro  wakati wakitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam saa 2 usiku katika barabara kuu ya Morogoro-Dodoma eneo la Bwawani.
Pia Machi 30, mwaka wabunge hao mchana saa saba waliwapokelewa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH),wakitokea hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro.
Na baadaye kuhamishiwa katika taasisi ya MOI kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya kibingwa.
Wabunge hao waliopata ajali ni Haji Ameir Haji (Makunduchi), Khamis Ali Vuai (Mkwajuni), Bhagwanji Maganlal Meisuria (Chwaka), Makame Mashaka Foum (Kijini), Juma Othman Hija (Tumbatu).

Akizungumza na mwanishi wa habari hizi Dar es Salaam jana Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Ustawi wa Moi, Almas Jumaa amesema mbunge Haji Ameir Haji yupo ICU akipatiwa matibabu.
Mkuu huyo wa kitengo cha mawasilia amesema  wabunge wengine wamesharuhusiwa baada ya hali zao kutengamaa. 
"Wanaendelea vizuri na leo (jana),tulikuwa na Kamati ya Amani kutoka  Zanzibar  pamoja na Naibu Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson  walikuja kuwatembelea," amesema. 
Ameongeza kuwa wabunge wengine watatu wameruhusiwa na kwamba wamebaki wawili  ambapo  Juma Othman Hija anaendelea na matibabu katika wodi ya kawaida.
Mkuu wa kitengo hicho aliwataja wabunge walioruhusiwa kuwa ni Khamis Ali Vuai, Bhagwanji Maganlal Meisuria , Makame Mashaka Foum.

No comments:

Post a Comment