Thursday, 12 April 2018

Amani Jamhuri ya Afrika ya Kati yatetereka


Rais Faustin-Archange Touadera 
RAIS wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadera ameyashutumu makundi ya wapiganaji yanayopambana na walinda Amani wa Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui.
Touadera amesema makundi hayo yamekuwa wakifanya uhalifu, hali iliyosababisha watu wengi kukamatwa mateka.
Siku ya Jumapili vikosi vya jeshi vya Umoja wa Mataifa vilianza operesheni yake kuwanyang'anya silaha wanamgambo ambao wanadhibiti baadhi ya maeneo katika mji mkuu wa nchi hiyo.
Mmoja wa walinda amani hao wa Umoja wa Mataifa ameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Mapema juzi Jumanne mamia ya waandamanaji wenye hasira waliilaza miili ya watu 16 mbele ya ofisi ya vikosi hivyo vya Umoja wa Mataifa mjini Bangui.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema vikosi vyao vimekuwa vikilenga makundi ya wahalifu na kukanusha taarifa kwamba wamekuwa wakishambulia raia.

No comments:

Post a Comment