Thursday, 19 April 2018

Anayeshukiwa kulipua majengo pacha ya Newyork Marekani akamatwa


Majengo pacha ya Newyork yaliyoteketea kwa moto Septemba 11, mwaka 2001


WANAMGAMBO wa Kikurdi wanaofanya kazi ya kulinda amani Kaskazini mwa Syria wanasema wamemkamata mtu mmoja mzaliwa wa Syria mwenye uraia wa Ujerumani ambaye anashukiwa kuwasaidia wanamgambo wa al-Qaeda kupanga mashambulizi ya Septemba 11 nchini Marekani, mwaka 2001.
Msemaji wa vikosi vya Kikurd amesema kuwa Mohammed Haydar Zammar amekuwa akifanyiwa mahojiano tangu alipokamatwa.
Zammar anashutumiwa kuwa ndiye kielelezo muhimu katika shambulizi la uwanja wa Hamburg katika jela nchini Ujerumani miaka ya 1990 wakati Mohammed Atta na wengine walipopewa kazi maalum kisha kufundishwa kazi ya urubani na hatimaye kuruka na kuzielekeza ndege zao katika jengo pacha la kibiashara la World Trade Center na Pentagon.
Zammar alikamatwa pia nchini Morocco mwaka 2001 na akapeleka Syria lakini serikali ya Damascus ilimuachia huru baada ya kubadilishana na mfungwa mwenye msimamo mkali.

No comments:

Post a Comment