Saturday, 14 April 2018

Baini nguvu ya tangawizi ni kinga na msaada kwa maradhi mengi


Hii ndiyo tangawizi

TANGAWIZI ni kiungo kinachoweza kutumika katika mboga na vyakula vingine vya aina mbalimbali kwa kuwa inaongeza radha nzuri inayochochea mlaji kupenda kula au kunywa.

Tafiti mpya zionesha namna mmea huu ulivyo muhimu kwa afya ya binadamu ukihusisha uwezo wake wa kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali ya kiafya.

Kiungo au chakula hiki kinasaidia wenye matatizo ya tumbo, uvimbe, koo, kuharisha, mafua, baridi, tezi la shingo, maradhi ya kipindupindu na kuchelewa kupata siku za hedhi kwa wasichana.

Unaweza kuitumia baada ya kuichemsha na kunywa ikiwa bado ya moto. 

Kumbkumbu zinaonesha kuwa Serikali ya Marekani iliiorodhesha tangawizi kwa mara ya kwanza kama dawa kwa ajili ya binadamu kati ya mwaka 1820 na 1873.

Kiungo hiki pia huongezwa kwenye vinywaji na vyakula vingi vya viwandani zikiwemo soda, juisi na biskuti ili kupata radha nzuri zaidi.

Hata hivyo, mwenye tatizo ambalo linahitaji kutumia tangawizi ni vema aje makao yetu makuu ambapo atapata maelezo ya kina ya namna sahihi ya kuitumia. 

Mchanganuo huu umeletwa kwako na mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment