Sunday, 22 April 2018

Bashar al-Assad arudisha tuzo aliyopewa na Ufaransa


          
Bashar al-Assad
SYRIA imerejesha kwa Ufaransa tuzo ya Légion d'honneur aliyopewa rais Bashar al-Assad, ikisema kuwa haiwezi kuchukua tuzo kwa taifa ambalo limekuwa 'mtumwa' wa Marekani.
Hatua hiyo inajiri siku moja baada ya Ufaransa kusema kuwa adhabu ya kuikataa tuzo hiyo inakaribia.
Ufaransa hivi majuzi ilijiunga na Uingreza katika kuishambulia Syria kufuatia madai ya kutumia silaha za kinyuklia dhidi ya raia wake.
Tuzo hiyo ilirudishwa Ufaransa kupitia balozi ya Roma mjini Damascus.
Rais Assad alipewa tuzo hiyo ya hadhi ya juu 2001 baada ya kuchukua mamlaka kufuAtia kifo cha babake.
''Wizara ya masuala ya kigeni imerudisha kwa Jamhuri ya Ufaransa tuzo ya Légion d'honneuri aliopewa rais Assad'', wizara ya kigeni nchini Syria imesema katika taarifa.
''Sio heshima kwa rais Assad kuvaa tuzo iliyotolewa na taifa la utumwa na mshiriki wa taifa la Marekani linalounga mkono ugaidi'', iliongeza taarifa hiyo.
Takriban watu 3,000 kila mwaka hutuzwa tuzo hiyo ya hadhi ya juu kwa huduma waliyotoa kwa Ufaransa ama kwa kutetea haki za kibinaadamu, uhuru wa kujieleza ama sababu kama hizo.
Marekani , Uingereza na Ufaransa zilishambulia vifaa kadhaa vya serikali ya Syria siku ya Jumamosi ili kujibu matumizi ya silaha za kemikali katika mji wa Douma, ambao ndio mji wa mwisho uliokuwa ukikaliwa na waasi katika jimbo la Mashariki mwa Ghouta nje ya Damascus.
Zaidi ya watu 40 walifariki katika shambulio hilo la Aprili 7 kulingana na wanaharakati wa upinzani, wafanyakazi wa uokoaji na maofisa wa matibabu.
Serikali ya Syria imekana kutumia silaha za kemikali na kusema kuwa shambulio hilo lilipangwa. Viongozi wengine waliopewa tuzo hiyo ni pamoja na aliyekuwa rais wa Tunisia Zine El Abiine Ben Ali 1989 na rais wa Urusi Vladimir Putin 2006.
Kufikia sasa ni rais mmoja pekee aliyepokonywa taji hilo-rais wa Panama Manuel Norriega. Hivi majuzi Nyota wa Hollywood Harvey Weinstein pia alipokonywa tuzo hiyo baada ya kukabiliwa na mashtaka ya unyanyasaji wa kingono.

No comments:

Post a Comment