Thursday, 19 April 2018

Bilioni 1.9 zatengwa Ubungo kuwakopesha kinamama, walemavu
Meya wa Manispaa ya Ubongo, Boniface Jacob akizungumza wakati wa hafla fupi ya kusaini makubaliano na benki ya CRDB ambako mikopo hiyo itapitia.

Peter Simon

HALMASHAURI ya manispaa ya Ubungo, Dar es Salaam imetenga sh. bilioni 1.9 kwa ajili ya mkopo wa kinamama na vijana.

Hayo yalibainishwa jana April 18, 2018 na meya wa manispaa hiyo, Boniface Jacob wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano na benki ya CRDB ambapo mikopo hiyo itatolewa kupitia benki hiyo.

Meya Jacob ametoa mwito kwa vijana kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo kwani idadi yao imeonekana kuwa ndogo huku mkopo huo ni nusu wao na nyingine kwa kina mama na asilimia  20 inakwenda kwa walemavu.

"Nikiwa Manispaa ya Kinondoni tulitenga sh. milioni 800 kwa ajili ya mikopo kama hii, lakini halmashauri ya manispaa ya Ubungo ina muda wa mwaka mmoja na nusu tu lakini unaweza kuona kiasi tulichotenga kwa ajili ya mikopo kwa vijana na kinamama, ni kwa sababu tuko ‘commited’ kuwasaidia wananchi wa Manispaa ya Ubungo," amesema .

Manispaa ya Ubungo  itakuwa ya kwanza kwa utekelezaji wa agizo kwamba asilimia 20 ya fedha ni kwa ajili ya walemavu.

Kwa taarifa ya mratibu wa mchakato huo, Wanawake waliojitokeza  ni 11,321, vijana idadi yake ikiwa ni 1124 tu.

No comments:

Post a Comment