Saturday, 7 April 2018

Bilioni 5/- zimetumika ujenzi ukuta mgodi wa Tanzanite- BusunguUkuta unaozunguka mgodi wa Tanzanite.

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Martin Busungu amesema sh. bilioni 5 zimetumika katika ujenzi wa ukuta wa mgodi wa Tanzanite ulioko Mererani mkoani Manyara.

Jenerali Busungu amesema ukuta huo wenye kilometa 24.4 unazunguka eneo lote la mgodi wa Tanzanite na tathmini ya awali, ilionesha kuwa ni kilometa 21 na kwamba zingetumika sh. bilioni 4.

Akizungumza jana Aprili 6, 2018 katika uzinduzi wa ukuta huo, Busungu amesema vikosi 20 vya JKT vimejenga ukuta huo.

“Tumetekeleza kwa uadilifu na uamnifu ujenzi huu. Tunatoa shukran za dhati kwa taasisi za uhandisi Tanzania kwa ushirikiano  wao,” amesema

Ameongeza kuwa JKT ipo tayari kutekeleza maaagizo yoyote yakatayotolewa kwa mustakabali  wa Taifa.

“Hata hivyo, kulikuwa na changamoto kadhaa ikiwamo  ugumu wa ujenzi hasa katika miamba, uwepo njia nyingi za maji ambazo hata hivyo wahandisi  wa Pangani River walisaidia,” amebainisha.

Jana Rais Dk. John Magufuli alizindua ukuta huo.  Viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa mikoa, wilaya na mawaziri walihudhuria hafla hiyo ya kihistoria.

No comments:

Post a Comment