Saturday, 7 April 2018

Chenge awajia juu wabunge kuhusu kuzingatia kanuni


Andrew Chenge

Mwandishi Wetu, Dodoma

MWENYEKITI wa Bunge, Andrew Chenge amewajia juu wabunge kwa kuwataka wazingatie kanuni na taratibu za Bunge wawapo katika vikao vyao bungeni mjini Dodoma.

Chenge alitoa kauli hiyo jana bungeni mjini Dodoma wakati akijibu mwongozo wa mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga (CCM), aliyeomba mwongozo wa kiti chake ambapo alitaka Serikali itoe tamko la kupiga marufuku matumizi ya nembo ya taifa yenye picha ya mume na mke aliyevaa wigi hadi marekebisho ya picha hiyo yatakapofanyika.

Katika mwongozo wake Mlinga alidai kuwa katika nembo hiyo ya Taifa kuna picha ya bibi na bwana ambaye amevaa lubega na hivyo kuasi maisha halisi na desturi za Mtanzania lakini mwanamke huyo amevaa wingi haijulikani iwapo ni mwarabu au mzungu.

“Bibi amevaa wigi haendani na uhalisia wa Mtanzania, haakisi maisha halisi ya Mtanzania, haijulikani kama ni Mwarabu au Mzungu, ninaiomba Serikali isitishe matumizi ya nembo hiyo, hadi pale itakapofanyiwa marekebisho?," alidai Mlinga.

Goodluck Mlinga

Akijibu mwongozo huo, Chenge alihoji iwapo tukio hilo lilikuwa limetokea jana hadi mbunge huyo akafikia hatua ya kuhoji Narudia kwenye kanuni je, suala hili limetokea leo (jana) na kama halijatokea leo halipo kwenye kanuni, wabunge mnatakiwa kuheshimu sheria inayosimamia nembo ya taifa," alisema Chenge.

No comments:

Post a Comment