Sunday, 22 April 2018

Chukua tahadhali kuepuka vidonda vya tumbo


Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallaha Mandai akisisitiza jambo wakati akizungumzia umuhimu wa jamii kuchukua tahadhali dhidi ya vidonda vya tumbo akiwa ofisini kwake makao makuu Ukonga, Mongo la Ndege, Dar es Salaam.


VIDONDA vya tumbo ni miongoni magonjwa tishio yanayowakumba watu wengi na hivyo kuwafanya muda mwingi wahangaikie tiba badala ya kufanya kazi za kuwaongezea kipato katika familia na taifa.

Kulingana na tafiti inaonesha kuwa mtu mmoja kati 10 atakuwa anaugua vidonda vya tumbo licha ya kuwa tafiti nyingine zinabainisha kuwa miongoni mwa watu watano mmoja ameathirika na maradhi hayo.

Mtaalam wa tiba, lishe na rutubisho, Abdallah Mandai anasema vidonda vya tumbo vimegawanyika katika sehemu kuu mbili, vidonda vya ndani ya tumbo au sehemu ya juu ya utumbo mdogo.

Vidonda vinavyotokea katika utumbo ndiyo maarufu zaidi ambavyo huwapata zaidi wanaume na vidonda vya ndani ya tumbo huwashambulia wote wanaume na wanawake.

Mtaalam Mandai anasema chanzo cha ugonjwa huo ni baada ya chakula kinapoingia tumboni ili kusagwa, tumbo huzalisha majimaji ya aina mbalimbali yakiwemo ya asidi ambayo hufahamika kama saidi hidrokloriki.
"Asidi hii huanza kula kuta za tumbo aina zote mbili za vidonda vya tumbo hutokea kutokana na kutolingana nguvu kati ya nguvu ya mnyunyizo wa asidi ya tumbo katika kushambulia na uwezo wa kuta za tumbo katika kuzuia mashambulizi," anasema.
Tabibu huyo aliyepata uzoefu kutoka katika nchi kadhaa za Afrika, anasema kutokea vidonda vya tumbo kunategemea zaidi vipengele viwili.

"Kwanza, vitu ambavyo vinaongeza mnyunyizo wa asidi katika tumbo, mfano vyakula vya kusisimua, vya mafuta, uvutaji sigara, utumiaji wa pombe, chai, kahawa na baadhi ya dawa kama corticostisteroids, caffeine na reseprine.

"Pili, udhaifu wa ute na kuta za tumbo kuzuia ushambuliaji wa asidi. Katika kutibu vidonda vya tumbo, mara nyingi ni lazima kuongeza kinga ya ute au kupunguza uzalishaji wa asidi," anasema.

Mandai anatanabaisha kuwa mfadhaiko wa akili utokanao na shida za maisha ni moja ya vipengele vinavyosababisha vidonda vya tumbo.

Anafafanua kuwa mfadhaiko huo unaongeza utiririkaji wa asidi ndani ya utumbo. Hii asidi ya ziada ambayo hutiririka ndani ya tumbo imetengenezwa kwa ajiri ya kukisaga chakula chochote haraka iwezekanavyo.

"Lakini kama hakuna chakula cha kufanyiwa kazi, asidi hii humomonyoa kuta za tumbo na hivyo kusababisha vidonda.

"Utafiti uliofanywa katika miaka ya hivi  karibuni umeonesha kuwa akili hutumia nguvu nyingi katika mwili. Baadhi ya madaktari wamesema mfadhaiko huchangia sana kutokeza magonjwa," anasema.

Aidha, anataja dalili tisa za ugonjwa huo kuwa ni pamoja na kujisikia huzuni kupita kiasi hadi kupoteza matumaini yoyote, kupoteza kabisa uwezo wa akili kufurahi, kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa na pia kutokuwa na hamu ya kula ya chakula.

Anasema dalili nyingine ni mtu kukosa usingizi, wasiwasi unaosababisha hali ya kutotulia pamoja, kushindwa kukumbuka na kuamua, kukasirishwa na vitu vidogo, kujiona hana thamani na kujitenga na marafiki au ndugu.

Mtaalam Manda anasema watu waepuke uvutaji sigara, matumizi ya dawa bila ushauri wa wataalamu wa tiba kwa kuwa zipo zenye kemikali zinapotumiwa bila mpangilio unamweka mtumiaji katika hatari ya kupata magonjwa.

Aidha, anasisitiza wanajamii kuzingatia mlo kwani njaa ya muda mrefu inamweka mtu katika hatari ya kupata ugonjwa huo.

"Mwito wangu tu kwamba mtu asitumie dawa bila maelezo kutoka kwa wataalam kwa sababu baadhi zina kemilika zinapotumiwa bila ushauri zinaweza kumweka mtu katika uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo.

"Pia mvutaji wa sigara anaweza kupata ugonjwa huu, tena sigara inasababisha magonjwa mengi hata TB hivyo wavutaji waache kuvuta sigara," anasisitiza.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vinavyozalishwa na kampuni yetu.

No comments:

Post a Comment