Tuesday, 17 April 2018

Chuo cha Uongozi wa Mahakama - Lushoto (IJA) chakutana na wadau kujadili namna ya kujiboresha


Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA), Jaji mstaafu, John Mrosso akizungumza jambo na wadau walioshiriki kikao hicho, katikati anayemwangalia ni Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, kushoto ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Ferdinand Wambali.


Wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo, alipokuwa akielezea kuhusu chuo hicho.Washiriki wakifuatilia kwa makini mada zilizotolewa ambapo waliahidi kwenda kuzifanyia kazi ili kuboresha mafunzo yanayotolewa na chuo hicho kwa manufaa ya watumishi wa mahakama na wananchi kwa ujumla.


Kikao hicho kimewashirikisha wajumbe miongoni mwao wawakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo cha Magereza-Kiwira, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Ofisi ya Utumishi na Utawala Bora na Chuo cha Kodi. Aliyeketi nyuma wa kwanza kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo-Mahakama ya Tanzania, Shaaban Lila.


Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamis Juma akifungua kikao cha wadau kujadili kazi ya ulinganisho wa chuo cha uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA) na vyuo vingine vya mafunzo endelevu. 

Kikao hicho kati ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama na wadau wa vyuo vingine vinavyotoa mafunzo endelevu kimelenga kujadili uzoefu na nafasi ya ushirikiano wa karibu baina ya chuo hicho na vyuo vingine vya umma vinavyotoa mafunzo endelevu kwa watumishi wa umma na wadau mbalimbali katika sekta ya sheria, kikao hicho kilifanyika jana Aprili 16 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.


Picha ya pamoja ya washiriki; aliyeketi katikati ni Jaji Mkuu Profesa. Ibrahim Hamis Juma, wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA), Jaji mstaafu John Mrosso, wa pili kushoto ni Jaji wa mahakama ya rufani ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo-Mahakama ya Tanzania, Shaaban Lila, wa kwanza kulia ni Jaji Kiongozi, Mahakama Kuu ya Tanzania, Ferdinand Wambali na wa kwanza kushoto ni Jaji Dk. Paul Kihwelo, Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto (IJA).
(PICHA NA MARY GWERA, MAHAKAMA)

No comments:

Post a Comment