Wednesday, 25 April 2018

DC awafananisha wanawake na viwandaYeremias Ngerangera, Namtumbo

MKUU wa wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma, Luckness Amlima amesema wanawake ni viwanda kutokana na kazi ya uumbaji ambayo Mungu ameiweka kupitia miili yao hivyo wanapaswa kuheshimiwa.

Ametoa kauli hiyo jana katika viwanja vya shule ya sekondari Nasuli iliyopo mjini Namtumbo wakati  wa ufunguzi wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango ya kizazi (HPV).


Lackness Amlima

Akizungumza na wanafunzi  wa shule hiyo, Amlima amesema wanawake  ni viwanda kutokana na kazi ya uumbaji inayofanywa kuoitia miili yao kutoka kutungwa mimba hadi kuzaliwa mtoto.

Aidha,  kuelekea uchumi wa viwanda mkuu wa wilaya hiyo amewataka wanawake kupata chanjo ya kukinga saratani ya kizazi  ili kuzuia saratani  ya mlango wa kizazi  itakayowafanya waweze  kuendelea kuwa viwanda wa kuunda familia yenye afya bora.

Mganga mkuu wa wilaya ya Namtumbo, Yuna Hamisi amesema chanjo ya kuzuia  saratani ya mlango wa kizazi wilayani Namtumbo itaanza kwa kuchanjwa wasichana wenye umri wa miaka 14.

Yuna amefafanua kuwa utafiti uliofanywa na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO), limebaini kuwa wanawake ndio waathirika wakubwa wa saratani ya mlango wa kizazi  na serikali inaendelea na jitihada ya kutoa chanjo ili kuzuia saratani ya mlango wa kizazi.

Hata hivyo, amewataka wananchi kufahamu kuwa chanjo hiyo ni salama kwa afya kwa kuwa zimefanyiwa utafiti wa kutosha.

Mratibu  wa chanjo wa wilaya ya Namtumbo, Ahmedi Makando amesema chanjo hiyo itatolewa na watalaamu wa afya katika shule na vituo vya afya  na kuwataka walimu katika shule husika kutoa ushirikiano wakati wa mchakato huo endelevu.

No comments:

Post a Comment