Wednesday, 11 April 2018

Diamond Platinum kutembea na warembo wakali, siri yafichuka, wamo Wema, Joketi, Uwoya, Hamisa na Zari

Jipu pwaa! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kuvuja kwa siri inayodaiwa kuwa ndiyo chimbuko la staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa ‘mtundu’ wa watoto wa kike!


Mwanafamilia mmoja ambaye aliomba hifadhi ya jina, alivujisha ubuyu mpya wakati kukiwa na madai ya jamaa huyo kurudiana na aliyewahi kuwa mwandani wake, Wema Isaac Sepetu kwamba, watu wamekwa wakimshangaa Diamond kuwa na ‘totoz’ nyingi pasipo kujua chanzo chake.

“Unajua wengi wamemuona Nasibu (Diamond) ukubwani, wanafikiri hii michezo kaanza leo, hawajui tu, Nasibu tunayemjua sisi, ameanza michezo hii siku nyingi tu sema wengi walishindwa kujua labda kwa sababu hakuwa maarufu,” alisema ndugu huyo.


Diamond na Penny.
Akiendelea kushusha madini mbele ya kinasa sauti cha Ijumaa, ndugu huyo wa Diamond alisema kuwa, mkali huyo wa Bongo Fleva anaonekana kuirithi tabia hiyo kutoka kwa babu yake.
“Huyu atakuwa amerithi haya mambo ya warembo kutoka kwa babu yake. Maana babu yake naye alikuwa hivihivi.

“Babu ya (mzee Jumaa) alikuwa mtu fulani ambaye alikuwa akijijali sana hivyo hata wanawake nao walikuwa wakimpenda kutokana na muonekano wake,” anasema ndugu huyo.


Jokate.

Kama hiyo haitoshi, ndugu huyo alienda mbali zaidi kwa kubainisha kuwa, siku zote maji hufuata mkondo kwani mbali na babu yake, hata baba yake mzazi Diamond (Abdul Jumaa) naye alifuata mkondo huo.

We’ enzi za ujana wake baba Diamond alikuwa baba Diamond kweli. Alikuwa anajipenda, mtu smati hivi na michezo ya kurukaruka na warembo alikuwa nayo sana.

“Wewe mtazame baba Diamond hata sasa hivi tu, licha ya uzee alionao, lakini popote utakapomkuta, lazima atakuwa kapendeza, wakati mwingine anapiga hadi cheni na nini utadhani bado kijana,” anasema ndugu huyo.


Wema.
Amesema kama familia, mara nyingi wanapomuona Diamond mara yupo na huyu, mara yupo na mrembo mwingine, hawashangai sana maana wanafahamu asili yake.

“Watu waliomfahamu Diamond akiwa msanii ndiyo wanaweza kushangaa, lakini kwa sisi tunaofahamu zaidi asili yake, hatushangai kabisa,” alisema ndugu huyo.

Katika mahojiano hayo maalum, ndugu huyo alisema kuwa, wao kama ndugu, wanamuombea tu Diamond apate mtu sahihi ili atulie kwani hata kwa baba na babu yake, walipopata mtu sahihi walitulia na kufanya maisha.

“Wewe si unamuona hata baba Diamond, tangu alipoachana na mama Diamond, kwa sasa ametulia kabisa. Starehe yake kubwa sasa hivi ni bia kidogo basi,” alisema ndugu huyo.


Wolper.

Msururu wa warembo

Mkali huyo anayetamba na Wimbo wa African Beauty aliomshirikisha Omario wa Marekani, ana rekodi baab’kubwa ya kutembea na warembo maarufu wasiopungua 17.
Listi ya warembo hao ambayo haipo katika mpangilio maalum ni pamoja na Irene Uwoya, Wema Sepetu, Hamisa Mobeto, Jokate Mwegelo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Nuzrat.

Wengine ni Natasha wa Moyo Wangu, Rehema Fabian na Jacqueline Wolper, Tunda Sebastian, Lyn (Irene wa Kwetu), Najma na Hamisuu Malick.


Tunda.
Diamond anavyojinasibu

Mara kadhaa katika mahojiano yake na vyombo vya habari, Diamond amekuwa akijinasibu kuwa amekuwa ‘akiwatafuna’ warembo mbalimbali maarufu kwani kabla ya kuwa staa, walikuwa wakimdharau na kumuita majina ya ajabuajabu.

Anasema kuwa, baada ya kupata umaarufu na mkwanja, kweli ameamua kuwapitia warembo tofauti ili kukamilisha furaha ya moyo wake kwani ni ndoto aliyokuwa akiiota siku nyingi.


Uwoya.
Baba Diamond atia neno

Alipoulizwa kuhusu suala la ukoo wao kuwa ni watundu na watanashati, baba Diamond alikiri kweli wao ni watu watanashati na kwamba suala la wanawake kuvutiwa nao liko wazi, lakini haimaanishi kwamba ni watundu.

“Kuvaa kweli, tunavaa vizuri. Hilo la kwamba sisi ni watundu ni watu tu wanasema, lakini hatupo hivyo bwana,” anasema baba Diamond.
Kwa kuwa, Diamond tayari ameshazaa watoto wawili na Zari, anapaswa kusaka mtu sahihi ili aweze kufanya naye maisha kwani umri nao unamtupa mkono.
Stori: Mwandishi wetu

Kutoka JMABULA GLOB.

No comments:

Post a Comment