Thursday, 26 April 2018

Dodoma ni jiji kuanzia leo - Magufuli


Jiji la Dodoma

Mery Meshack, Dodoma

RAIS Dk. John Magufuli ameitangaza rasmi manispaa ya Dodoma kuwa jiji kama yalivyo majiji mengine ya Tanga, Mbeya, Arusha, Mwanza na Dar es Salaam.

Rais Magufuli ametoa tangazo hillo leo wakati akihutubia kwenye sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,  zinazofanyika kwenye uwanja wa Jamuhuri mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watanzania na viongozi mbalimbali wakiwemo wastaafu.

“Kuanzia leo kwa mamlaka mliyonipa Dodoma ni jiji. Dodoma ni jiji. Na Mkurugenzi wa hapa kuanzia leo anakuwa Mkurugenzi wa jiji la Dodoma,” amesema Rais Magufuli.

Wakati huo huo Rais Magufuli amesisitiza wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara kuulinda muungano huo wenye histori na mfano wa kuigwa duniani.

No comments:

Post a Comment