Thursday, 19 April 2018

Epuka vichocheo vya ugonjwa wa Kisukari kuulinda mwili wako


Mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akizungumzia namna bora ya maisha iipasayo jamii kuishi ili kuepukana na maradhi ya kisukari. 


UGONJWA wa Kisukari ni miongoni mwa magonjwa yasiyoambukiza lakini ni tishio zaidi hasa katika kizazi cha sasa. Ni tishio kwa sababu watu wengi tena wa jinsia na rika zote wanakabiliwa na tatizo hilo huku idadi kubwa ya watu wengine wazima wakiwa hatarini kukumbwa nao.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Kisukari ya Kimataifa mwaka 2009, ulibaini watu milioni 344 duniani wako katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari. Taasisi hiyo pia ilitangaza kuwa, watu milioni 285 tayari wanasumbuliwa na ugonjwa huo duniani kote.

Utafiti huo unabainisha tatizo hilo nchini na duniani kuwa ni kubwa na kwamba kuna kila sababu ya jamii kuchukua hadhali dhidi ya ugonjwa huo kwa kuepuka vichocheo.

Kisukari ni ugonjwa unaotokea pale mwili unaposhindwa kusaga vema chakula ili kutoa nishati na kusaidia ukuaji wa mwili. Chakula kinapoliwa husangwa na kubadilishwa kuwa glukosi. Glukosi ni aina ya sukari kwenye damu ambayo ndio chanzo cha nishati au kama mafuta kwa ajili miili yetu.

Baada ya chakula kuyeyushwa hushika njia kuelekea katika damu. Seli za mwili hutumia glukosi kama chanzo cha nishati. Hata hivyo, glukosi haiwezi kuingia katika seli za mwili bila kutumia wenzo unaoitwa insulini.

Insulini huwezesha seli za mwili kuchukua glukosi. Insulini ni homoni ambayo inatengenezwa na kongosho au pancreases.

Baada ya kula chakula, kongosho hutoa kiasi cha kutosha cha insulini kinachoweza kuhamisha glukosi iliyoko kwenye damu kwenda kwenye seli, na kwa njia hiyo kiwango cha sukari katika damu kinapungua.

Mtu mwenye kisukari kiwango cha sukari katika damu yake kinakuwa juu sana. 

Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho Abdallah Mandai anasema watu wachache huzaliwa na tatizo hilo huku wengine hupata matatizo hayo kutokana na aina ya vyakula na maisha yao ya kila siku.

"Kutumia sukari nyingi pamoja na mafuta mengi katika vyakula na vinywaji, kutofanya mazoezi, kunywa pombe kupita kiasi na kuvuta sigara kunaongeza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kisukari baada ya miaka ya ujana,"anasema mtaalam Mandai.

Pia anasema ugonjwa huo ni mlolongo wa matatizo ya muda mrefu na mfupi kutokana na upungufu au kutoweza kutumika vizuri kwa kichocheo kinachoitwa insulini. Kichocheo hicho hutengenezwa na chembechembe zilizopo ndani ya kiungo cha kongosho.

"Miili yetu inahitaji insulini ili kuweza kutumia sukari tuliyo nayo mwilini. Sukari inatokana na chakula ambacho tunakula kila siku na hutumika kwa kutupa nguvu mwilini. Kwa kawaida sukari ikizidi ya ziada inahifadhiwa katika ini kama mafuta,"anabainisha.

Anasema mafuta hayo hubadilishwa na kuwa sukari na kutumika wakati kukiwa na njaa kwa muda mrefu.

Anasema endapo kuna matatizo ya kutengeneza au kutumika kwa insulini, sukari mwilini huongezeka haraka na inamaanisha ugonjwa wa kisukari upo na dalili huanza kuonekana.

Mandai anasema vipo vichocheo vya wazi ambavyo vinamweka mtu katika hatari ya kupata ugonjwa huo miongoni mwavyo ni pamoja na unene uliozidi na kiribatumbo (kitambi).

Pia ulafi, baadhi ya dawa za kizungu, msongo wa mawazo, historia ya ugonjwa ndani ya familia, tezi ya shingo, kutofanya mazoezi, umri wa zaidi ya miaka 40 ambapo kongosho lake linapungua uwezo kutoa insulini hivyo kusababisha kisukari.

Zipo dalili nyingi za ugonjwa wa kisukari kwa mujibu wa mtaalam Mandai miongoni mwazo kuwa ni pamoja na kiu ya mara kwa mara, kupungua uzito licha ya kula vizuri na njaa kali ya mara kwa mara.

"Dalili nyingine ni jasho jingi, uchovu usioeleweka hata bila kufanyakazi, kizunguzungu, macho kupungua uwezo wa kuona na kidonda kisichopona haraka," anasema.

Anabainisha kuwa iwapo mtu atapata ugonjwa huo halafu akapuuza kwa kutokuutibu inavyostahili anakuwa hatarini kupata madhara mengi ambayo husababishwa na kiwango cha sukari kuwa cha juu zaidi mwilini.

Anatanabaisha kuwa magonjwa ya moyo, kiharusi, kupungua nguvu za kiume na figo kushindwa kufanya kazi ni miongoni mwa madhara ambayo anaweza kuyapata mwathirika wa ugonjwa wa kisukari.

"Wengi wanasema kisukari hakitibiki ni kweli kwasababu sukari ukitibu maana unaiondoa unaweza kumfanya mtu afe.

"Ninachofanya natoa kirutubisho kinachosaidia kuiamsha kongosho ambayo inafanyakazi ya kuunguza sukari isiyohitajika mwilini na kubakisha sukari ambayo inampa nishati na kumfanya mtu awe na nguvu," anasema.

Mtaalam huyo anatanabaisha kuwa ugonjwa huo ni kama magonjwa mengine ambayo kampuni yake sasa kinatengeneza virutubisho vyenye nguvu ya kusaidia kupambana nayo.

"Ninachofanya mimi naiamsha kongosho kupitia kirutubisho tiba. Kirutubisho hicho kina nguvu ya kuamsha na kuiimarisha kongosho ili iweze kufanya kazi yake ya kutema insulin na kumfanya mtu arudi katika hali yake ya awali," anasema.

Mandai anafafanua kuwa sanjari na kumsaidia mgonjwa husika kwa virutubisho pia anampa darasa la namna anavyoweza kutunza mwili wake usishambuliwe na magonjwa kwa kudhibiti ulaji.

“Chakula unachokula sasa ndicho uzima wako wa kesho,"anasema mtaalam huyo, "asubuhi kula kama mfalme, mchana kula kama malkia lakini jioni kula kama maskani utalinda mwili wako dhidi ya magonjwa,"anasisitiza.

Pia anaonya jamii ipende mazoezi na kuepuka kula sukari nyingi sanjari na unywaji pombe na uvutaji sigara kupita kiasi.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vinavyozalishwa na kampuni yetu.

No comments:

Post a Comment