Thursday, 26 April 2018

Epuka visababishi vinavyopunguza nguvu za kiumeMtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akizungumzia umuhimu kwa wanaume kuepuka viashiria vinavyopunguza nguvu za kiume.


TATIZO la upungufu wa nguvu za kiume linaonesha kuwaathiri wanaume wengi zaidi hapa nchini. Tatizo hilo limekuwa likiongezeka kila kukicha kutokana na sababu mbalimbali.

Ongezeko lake pamoja na mambo mengine linaelezwa kutishia kulegalega kwa ndoa nyingi huku nyingine zikiwa katika hatari ya kuvunjika kabisa.

Ndoa zinakuwa katika hatari hiyo kwa sababu moja ya muhimili wake ni wanandoa wawe na uwezo wa kushiriki tendo la ndoa ambalo linawaunganisha.

Hata hivyo, tatizo hilo limegawanyika katika makundi tofauti ambapo wapo walio pungukiwa nguvu na kushindwa kabisa kushiriki tendo la ndoa huku wengine wakiwa na uwezo mdogo kwa kushiriki mara moja tu.

Pamoja na sababu nyingine, Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai, anasema ulaji wa vyakula vya kisasa ambavyo vingi hukaangwa, ufanyaji kazi ngumu pamoja na uvutaji wa sigara huchochea ukubwa wa tatizo hilo.

Anabainisha kuwa yeye ana amini dawa ya 'moto ni maji' na si moto kama ilivyozoeleka.

Anasema wenye matatizo hayo wanatibiwa kwa mimea tiba ambayo ina uwezo wa kurutubisha mbegu za kiume.

"Ipo mmea tiba ambayo ina 'carolide' ya kutosha ambayo inasaidia tatizo hilo kwa kiasi kikubwa.

“Naomba sasa turudi katika tiba asili na matunda, tuache kupeperusha bendera ya umagharibi," anasema Mandai.

Anaongeza kuwa wafanyakazi wa migodini wapo katika hatari ya kukumbwa na tatizo hilo kutokana na kukaa kwao muda mrefu kwenye eneo lenye joto kali.

Anatanabainisha kuwa uvutaji wa sigara huchangia tatizo hilo kutokana na kwamba zina nikotini nyingi.

"Ninapogundua ana tatizo hilo nampa virutubisho ambavyo humwezesha kurudisha heshima yake ndani ya ndoa na nitamwelekeza namna ya kuishi na vyakula anavyotakiwa kula ili kuendeleza afya yake nzuri," anasema.

Mandai anasema matibabu kwa kutumia mimea hupenya ndani ya mbegu za kiume hivyo kuondoa kabisa tatizo hilo.

Licha ya kuwa na dawa za kuondoa tatizo hilo Mandai anasema wapo waliozaliwa na ulemavu wa kukosa nguvu za kiume (hanithi), watu hao kuwasaidia wanachangamoto kidogo.

Anabainisha kuwa matabibu wa zamani walikuwa na uwezo wa kuwatibu kundi hilo la watu.

Anasema si ajabu kusikia kwamba wanaume wengi wana tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kutokana na mazingira ya kazi na hasa matumizi ya vitendea kazi vinavyotumia mionzi kwa muda mrefu.

Imebainishwa na wataalamu wa magonjwa ya uzazi kwamba madereva wanaoendesha magari kwa safari ndefu wako kwenye hatari ya kuwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa kuwa kiti cha dereva huwa kina moto ambao humdhuru dereva endapo atawajibika katika kazi hiyo kwa zaidi ya saa 14 kwa siku.

Upungufu wa nguvu za kiume ambao unatibika kwa haraka ni ule utokanao na mazingira na matumizi ya vyakula ambavyo vinasababisha kuziba mirija ya damu hivyo inapohitajika mwili kusisimka kwa ajili ya tendo fulani iwe la tahadhari au la kushiriki ngono huwa kazi nyepesi.

Tatizo hilo ambalo hutokana na kurithi linaweza kutibika lakini kazi huwa kubwa ikilinganishwa na matibabu ya wanaotakiwa kuacha kutumia tumbaku au kula vyakula vyenye mafuta mengi.

No comments:

Post a Comment