Monday, 23 April 2018

Fahamu nguvu ya mkwaju katika kuzuia mimba kutoka


Mkwaju

UKWAJU ni tunda linalotokana na mkwaju. Mkwaju ni mti unaotoa matunda ambayo yanajulikana kama ukwaju ambayo wengi huyatumia kwa kula au kutengeneza juisi.

Bila shaka wengi hutumia tunda hilo lenye ladha ya ugwadu (uchachu) kwa kutengeneza juisi ambayo hutumika kama kinywaji kinachoburudisha.

Hata hivyo, matabibu wanatueleza kuwa mti wa mkwaju una faida nyingi kwa binadamu tofauti na wengi tunavyouchukulia.

Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai anasema mti huo una faida kuanzia mizizi, magome, majani na hata matunda yake.

Anasema unategemewa katika tiba za magonjwa mbalimbali yanayowakabili wanadamu wengi.

"Tukianza, mizizi ya mkwaju, ikitengenezwa vizuri ina uwezo wa kutibu magonjwa mengi likiwemo tatizo la mkojo mchafu (uti).

"Mizizi inasaidia sana kuzibua mirija ya uzazi pia humpunguzia mwanamke mauamivu wakati wa hedhi na wa tendo la ndoa," anasema. 

Aidha, anafafanua kuwa majani ya mkwaju yakiandaliwa vizuri yanasaidia kuzuia homa za mara kwa mara ukiwemo ugonjwa wa malaria, kuharisha damu, homa ya matumbo na vidonda vya tumbo.

"Pia majani ya mkwaju yakikaushwa kivulini kisha kupondwa na unga wake ukichanganywa na mafuta ya nazi unasaidia kuondoa magonjwa ya ngozi na mwasho.

"Kwa wenye matatizo ya miguu inayokufa ganzi au kuwaka moto wachanganye unga wa majani ya mkwaju na mafuta ya nazi kisha mgonjwa achue eneo husika maumivu yanaondoka kabisa," anasema.

Hali kadhalika anasema kwa wenye matatizo ya athma (pumu) unga huo ukichanganywa na asali kisha mgonjwa anapolamba inasaidia kuondoa hali hiyo pia kifua kikavu.

"Kama nilivyosema mti huu umesheheni faida, gome la ukwaju likianikwa kivulini na kisha kutwangwa unga wake unasaidia kwa kinamama wenye matatizo ya kifafa cha uzazi.

"Gome hilo linawasaidia pia wale wanawake wenye matatizo ya kuzaa watoto wafu na wale wanaobeba mimba na kutoka kabla ya wakati.

"Namna ya kuandaa tiba hii chuna vizuri gome la mkwaju, anika kivulini baada ya kukauka litwangwe vizuri, kwa kuwa masuala haya yanawahusu wanawake ni vema dawa hii akaiandaa mwanamke tena aliyekoma hedhi," anasema.

Anaongeza kuwa kulingana na imani ya tiba asili kwa sababu upande wa tiba hiyo una masharti ya maandalizi ya dawa.

Anafafanua katika mimea tiba kuna alcolide na anthraguinone kemikali inayopatikana katika mimea tiba yote hivyo anapoiandaa mwanamke asiyekoma hedhi ana harufu yenye uwezo wa kuiondoa kemikali hiyo.

Aidha, akiuzungumzia ukwaju (tunda) anasema ukitengenezwa juisi una faida nyingi katika mwili wa binadamu ikiwemo ni pamoja na kuongeza vitamini A, B na C.

"Nashauri mtu atumie juisi ya ukwaju daima. Ni vema mtu anywe mara mbili au hata mara tatu kwa siku. Kwanza inaongeza vitamini A, B na C lakini pia ina madini ya chuma, calcium na zink," anabainisha.

Anasema kwa wenye shida ya kupata choo, tumbo kuunguruma, watumie juisi hiyo itawasaidia kuondokana na changamoto hizo.

Mandai anatanabaisha kuwa juisi hiyo inasaidia kuweka uwiano wa sukari mwilini, lakini pia kinamama wanaonyonyesha huku wakikabiliwa na changamoto ya kutotoa maziwa ya kumtosha mtoto watumie juisi hiyo itachochea maziwa kutoka kwa wingi.

Kwa wanawake wenye changamoto ya kuwashwa sehemu za siri, anasema juisi ya ukwaju ikitumiwa ipasavyo inasaidia kuondoa tatizo hilo.

"Juisi hii akiitumia mama mjamzito ipasavyo itasaidia kujifungua bila upasuaji kwa kuwa itamwongezea kiwango kikubwa cha calcium ambayo inamwongezea nguvu," anasema mtaalam huyo.

Aidha, anaonya kuwa ni vema mtu mwenye moja ya changamoto tajwa akatumia dawa hizo baada ya kumwona mtaalamu ambaye atamwelekeza matumizi stahiki.

Anatoa mwito kwa Watanzania kutokata miti hovyo lakini pia waongeze kasi ya kupanda aina mbalimbali ikiwemo ya matunda kama mkwaju na mengine kwa kuwa ina faida nyingi ikiwemo kivuli.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho tiba vyetu.

No comments:

Post a Comment