Thursday, 26 April 2018

Hafla ya kuvalishwa cheo Mwambata wa JWTZ wa Ubalozi wa Tanzania nchini India, Brigedia Jenerali A. S Mwami

Balozi wa Tanzania nchini India, Baraka H. Luvanda akimvalisha cheo cha Brigedia Jenerali A.S Mwami ambaye ni Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini India.

Brigedia Jenerali A.S Mwami ni miongoni mwa maofisa wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambao Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dk. John Magufuli aliwapandisha vyeo Aprili 12, mwaka huu (2018). Awali Brigedia Jenerali Mwami alikuwa na cheo cha Kanali. Hafla hiyo fupi imefanyika katika Ubalozi wa Tanzania nchini India na  kuhudhuriwa na watumishi wa ubalozi huo.


Brigedia Jenerali A. S. Mwami akiwa kwenye picha ya pamoja na familia yake baada ya kuvalishwa cheo hicho.


Balozi Baraka Luvanda (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Brigedia Jenerali A.S Mwami baada ya kumvalisha cheo hicho.


Balozi Baraka Luvanda (wanne kutoka kulia) akiwa pamoja na Brigedia Jenerali A.S Mwami wakiwa katika picha ya pamoja familia ya Mwami na watumishi wa ubalozi wa Tanzania nchini India.

No comments:

Post a Comment