Thursday, 5 April 2018

Heche aunganishwa kwenye kesi ya kina Mbowe


Mbunge wa Tarime Vijiji, John Heche (katikati)

MBUNGE wa Tarime Vijiji, John Heche amesomewa mashtaka matatu katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam na kuunganishwa katika kesi inayowakabili viongozi 7 wa Chadema akiwemo mwenyekiti, Freeman Mbowe.

Wakili wa serikali, Faraja Nchimbi amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa wanaomba kumuunganisha Heche katika kesi inayowakabili wenzake ambapo yeye atakuwa mshtakiwa wa nane.

Hakimu Mashauri amekubali kumuunganisha, ambapo Wakili Nchimbi amedai Heche anakabiliwa na makosa matatu ikiwemo kufanya mkusanyiko ama maandamano yasiyokuwa halali.

Heche ameachiwa kwa masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya sh. milioni 20 kila mmoja, pia awasili kituo cha Polisi Kat (Central Police), kila Ijumaa. Kesi imeahirishwa hadi April 16, 2018.

No comments:

Post a Comment