Sunday, 8 April 2018

Hili ndilo embe lililosheheni vitamini kwa afya yako


Embe

EMBE ni tunda lenye ladha tamu na lina vitamin nyingi. Linatokana na mwembe (mti wa embe). Asili yake ni Asia Kusini.
Sasa tunda hilo ni kati ya matunda yanayovunwa kwa wingi zaidi Afrika Mashariki na ulimwenguni kote hususan katika nchi zenye hali ya hewa ya kitropiki.
Licha ya kuliwa bichi, pia linatumika katika mapishi mbalimbali ili kuongeza radha. Embe lililowiva linaliwa au kutengenezewa juisi tamu inayopendwa na watu wa rika zote.
Majani machanga ya mwembe yanapochumwa na kupondwa pondwa kisha kukaushwa na kupata unga mgonjwa wa kisukari atumie vijiko viwili vya chai katika uji kila siku kwa maisha yake yote. Tumia unga huu badala ya sindano.
Kama wakati wa msimu wa matunda ya embe mtu akala matunda hayo mengi wataalamu wanasema mwili wake unaweza kutunza vitamin C ambayo inaweza kutumika kidogo kidogo hadi msimu mwingine bila kuisha.
Ukitumia matunda mengi au mboga za majani, vitamini husika hutumika siku hiyo tu mwili hauwezi kutunza nyingine.
Ikiwa unakabiliwa na maumivu katika mwili kama mgongo na meno unaweza kutumia embe yaani ganda la pili kutoka la nje, ondoa hilo lichemshe kunywa au loweka unywe au chukua unga uliopondwa na ujaze katika tundu la jino linalouma litapata nafuu. Ni vema ukiponda kabla ya kutumia katika jino.
Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.
Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment