Sunday, 29 April 2018

Ijue nguvu ya kitunguu swaumu kwa tatizo la kiuno


Kitunguu swaumu

MAUMIVU ya kiuno yamekuwa yakiwatatiza zaidi watu wenye umri wa kuanzia miaka 30. Mara nyingi wanawake ndiyo husumbuliwa zaidi na maradhi ya kukaza au kuuma kiuno.

Kukaa vibaya kwa muda mrefu, kunyanyua vitu vizito au kuvibeba vibaya, kuvaa viatu vyenye visigino virefu, kutofanya mazoezi ya kutosha, matatizo katika kipindi cha hedhi na uzito mkubwa wa mwili miongoni mwa sababu zinachangia tatizo hilo. Unaweza kutibiwa kwa kutumia kitunguu swaumu na aloe vera.

Kitunguu swaumu

Tafuna punje sita za kitunguu swaumu kila siku, pia ponda nyingine moja ya ipake sehemu yote ya kiuno inayouma kabla ya kwenda kulala.

Aloevera

Kata kipande cha nusu futi cha jani la aloevera, parua na kuondoa rangi yote ya kijani iliyo juu ya jani, kata vipande vidogo tafuna na kumeza. Endelea na tiba hii kwa muda wa siku tatu hadi saba.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu.

No comments:

Post a Comment