Wednesday, 25 April 2018

Ijue nyanyachungu ilivyo na nguvu ya kukinga maradhi ya tumbo


Nyanyachungu

WATU wengi wanazipika nyanyachungu pamoja na aina nyingine za vyakula hususan mboga ili kuongeza radha, licha ya kuwa wapo wanaozitumia zenyewe kama mboga.

Nyanyachungu zinazalishwa kutoka katika mmea ambao hukua kufikia urefu wa mita moja hadi moja na nusu, matawi na majani yake hufanya kichaka.

Nyanyachungu zinaweza kuwekwa katika makundi mawili zinazotoa matunda madogo madogo na nyingine matunda makubwa na machungu kiasi. Sina uhakika ni kwanini zinaitwa jina hilo lakini huenda ni kutokana na kuwa na radha ya uchungu kiasi.

Rangi ya matunda ya mnyanyachungu (nyanyachungu) yanaweza kuwa ya kijani kibichi wakati mwingine kijani-njano, au njano-nyeupe wakati yakipevuka kabisa hugeuka kuwa na rangi nyekundu.

Nyanyachungu zikipevuka huwa hazifai tena kuliwa, ila kwa kutoa mbegu za kupanda.

Mmea wa nyanyachungu (mnyanyachungu) una uwezo wa kustahimili upungufu wa maji kuliko aina nyingine za mboga pia hushambuliwa na baadhi ya magonjwa yasababishwayo na mvua au unyevunyevu mkubwa.

Wakati wengi wakizitumia kama mboga, mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai anasema nyanyachungu zinasaidia sana kwa wanaosumbuliwa na maradhi ya tumbo.

Anasema kwenye nyanyachungu mna kiwango kikubwa cha madini lakini pia mna vitamini A, B na C.

Anabainisha kuwa kutokana na wingi wa vitamini na madini, nyanyachungu inatibu maradhi mengi yakiwemo ya matumbo.

Mandai anasema kwa wakazi wa maeneo ya baridi na Pwani mara nyingi husumbuliwa na maradhi ya tumbo na hivyo ni vema wakaitumia nyanyachungu kuepukana na maradhi hayo.

"Ndani ya nyanyachungu mna tiba au ni maajabu makubwa katika tiba. Mna vitamini A, B na C, lakini pia mna kiwango kikubwa cha madini.

"Kwa wakazi wanaoishi katika maeneo ya baridi na Pwani nawashauri watumie nyanyachungu kwa kiwango kikubwa kwa sababu mara nyingi wanakabiliwa na changamoto ya maradhi ya tumbo," anasema.

Anaongeza kuwa katika maeneo hayo wanawake na wanaume wengi wanasumbuliwa na maradhi ya tumbo kwa kiwango kikubwa zaidi.

Anatanabaisha kuwa kwa wanaume wanaosumbuliwa zaidi na tatizo la ngili sanjari na tatizo la tumbo kujaa gesi na kutopata choo vizuri watumie nyanyachungu.

Anasema mtu anaweza kujisikia tumbo limejaa isivyo kawaida hata kama hajala chochote, hali hiyo inaweza kupatiwa ufumbuzi kutokana na matumizi stahiki ya nyanyachungu.

"Nyanyachungu zinasaidia kupambana na magonjwa mbalimbali, tutumie chakula kuwa tiba badala ya dawa kuwa tiba, katika chakula ndani yake kuwe na mbogamboga na matunda kwa wingi.

"Nyanyachungu zinasaidia usanisi wa chakula, mzunguko mzuri wa damu bila tatizo lakini pia kumkinga mtu yeyote kutoshambuliwa na maradhi yakiwemo ya moyo.

Nyanyachungu ni tiba kuanzia majani, mizizi na matunda ambapo vinapotumiwa vizuri vinaondoa changamoto zote.

"Juisi ya nyanyachungu ni kinga ya maradhi mengi tusizitumie dawa kwa tiba bali mboga za majani kwa kujikinga na maradhi, tutumia mboga mboga kujikinga na maradhi.

"Tumejaliwa kupata mimea tiba ambapo ndani yake kuna mboga, ndani yake kuna matunda na ndani yake mna chakula cha aina nyingine ambazo zinahitajika katika miili yetu," anasisitiza Mtaalam Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vinavyozalishwa na kampuni yetu.

No comments:

Post a Comment