Monday, 23 April 2018

IS waua 57 kwa bomu kituo cha kujisajili wapiga kura


Mmoja wa watoto aliyeshambuliwa katika tukio hilo
WATU 57 wamefariki dunia katika shambulio la bomu la kujitoa muhanga lililolenga kituo cha kuandikishia wapiga kura katika mji mkuu wa Afghanstan, Kabul.
Taarifa kutoka mamlaka husika mjini humo zinasema kati ya watu hao waliouawa walikuwa katika mistari ya kujiandikisha. Miongoni mwao wamo wanawake 21 na watoto watano,huku wengine 119 wakijeruhiwa pia.
Kundi la kigaidi la Islamic State (IS) limejinasibu kuhusika katika shambulio hilo la kikatili.
Uandikishaji wapiga kura nchini humo umeanza mwezi uliopita ikiwa ni maandalizi kwaajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.
Taarifa kutoka ndani ya IS zinasema mtu aliyetekeleza shambulio hilo alikuwa amevalia mkanda wa vilipuzi na alikilenga kituo cha kujiandikishia cha eneo la Dashte Barchi Magharibi mwa Kabul.
Dashte Barchi eneo lenye idadi kubwa Waislam wa Kishia ambao wamekuwa wakilengwa na kundi la IS.
Watoto waliouawa katika shambulio hilo, walikuwa wamesimama pia katika mistari ya watu waliokuwa wanajiandikisha jana Jumapili asubuhi.
Mlipuko huo pamoja na kusababisha vifo lakini pia umeharibu magari  ambapo hadi sasa kumekuwa na mashambulio manne tangu kuanza uandikishaji huo wiki iliyopita.
Chanzo BBC.

No comments:

Post a Comment