Sunday, 22 April 2018

Jaffo azindua Magufuli Square, ataka Dodoma kuwa mji wa matunda


 Suleiman Jaffo

WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi, Suleiman Jaffo amewataka watendaji walio chini yake kuhakikisha wanawahimiza wananchi kupanda miti ya matunda ndani ya mkoa wa Dodoma sanjari na halmashauri ya manispaa ya Dodoma ili mji huo uwe wa matunda.

Kauli hiyo ameitoa mwanzoni mwa wiki kwenye Chuo cha Serikali za mitaa Hombolo wakati akizngumza na wanafunzi na wafanyakazi wa chuo hicho wakati akizindua mnara uliopewa jina la Magufuli Square kuenzi utendaji wake.

Amesema anataka kuona upatikanaji wa matunda kwenye mji wa Dodoma wanapande miti ya matunda kuanzia kwenye ili kuwa na mji wenye urahisi wa upatikanaji wa matunda ya aina mbalimbali.

“Nataka mtu akiwa na hamu na matunda wakati anatembea anaweza kuyapata popote ndani ya mji huu tena kwa urahisi kuliko kutembea umbali mrefu kutafuta ukwaju au maembe” amesisitiza Jaffo.

Akizungumzia mnara huo aliozindua amesema lengo lake ni kuhamasisha watumishi wa umma kujua wajibu wao katika utumishi na kujitathmini katika uwajibikaji wao na kutoa huduma bora kwa wananchi

Amesema kufanyakazi kwa bidii ndio msingi katika maisha yao ya utumishi na kujali hali za wananchi wanyonge wa taifa hili kama alivyo Raisi Magufuli ambaye amejipambanua kuwajali wanyonge wa nchi hii na sisi tujitazame kama tumefanana naye katika majukumu yetu ya kila siku.

Akautaka uongozi wa chuo hicho na wanafunzi kuanza kuishi kwa mitazamo ya kuwatumikia wananchi wanyonge kwa maslahi mapana ya kuweka mbele uzalendo kwa nchi yao ili kulipeleka taifa mbele kwenye mafanikio sahihi ya uchumi wa kati.

No comments:

Post a Comment