Saturday, 7 April 2018

JPM ampa kibarua IGP


Rais Dk John Magufuli

Peter Simon, Arusha

RAIS Dk. John Magufuli amemwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro kuhakikisha inapofika kesho (Aprili 8, 2018) awe ameshawaingiza askari Polisi walionguliwa moto nyumba zao hapo awali katika nyumba mpya ambazo zimezinduliwa leo.

Dk. Magufuli ametoa agizo hilo leo (Aprili 7, 2018) wakati alipokuwa anazungumza muda mchache baada ya uzinduzi wa nyumba za askari zilizojengwa mkoani Arusha.

Ametoa pole kwa majanga yaliyotokea ya kuunguliwa moto nyumba zao, huku akiwapongeza wadau mbali mbali waliojitolea kufanikisha ujenzi upya wa nyumba hizo.

"Nimepata mawazo ni kitu gani tunaweza kufanya kuhusina na matatizo ya nyumba za Polisi, sasa ninachoomba IGP wale walionguliwa nyumba, kesho waingie katika nyumba zao hizi mpya ambazo zimemalizwa kujengwa.

“Kwasababu najua muda mwingine wanaweza wakachomekwa Polisi wengine halafu waliokuwemo wakaambiwa hapana", amesema Dk. Magufuli.

No comments:

Post a Comment