Thursday, 5 April 2018

JPM mgeni rasmi uzinduzi nyumba za polisi ArushaMwandishi Wetu, Arusha

RAIS Dk. John Pohn Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa nyumba za polisi na vituo vyake jijini hapa.

Akizungumza na wanahabari Kamanda wa polisi mkoani hapa, DCP Charles Mkumbo amesema kutakuwa na uzinduzi wa vituo viwili cha Utalii na Diplomasia na kingine ni Kituo cha daraja la kati kilichopo Murieti jijini hapa.Kamanda Mkumbo amesema kutakuwepo pia na maonesho mbalimbali ya jinsi Jeshi la Polisi linavyofanya kazi za kuwahudumia wananchi ambayo yatafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid .

Amewataka wananchi kutokuwa na hofu kwani hali ya usalama jijini hapa 
imeimarishwa na amewaomba wajitokeze  kwa wingi katika sherehe hizo.

No comments:

Post a Comment