Thursday, 19 April 2018

JWTZ yatakiwa kujivunia mafanikio
ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kikosi cha 11 wametakiwa kujivunia mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi cha mwaka mmoja waliokuwa wakishiriki ulinzi wa amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan na kutunukiwa Nishani za Umoja wa Mataifa (UN).

Taarifa iliyotolewa na JWTZ nchini inasema, hayo yamebainishwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa (UNAMID)  jimboni humo, Luteni Jenerali Leonard Ngondi wakati wa sherehe za kuwatunuku Nishani askari wa JWTZ  katika sherehe zilizofanyika Khor Abeche.

“Kutunukiwa Nishani ni jambo la kujivunia kwa kuwa zimetolewa kwa sababu askari wamefanya kazi nzuri ambayo inapaswa kupongezwa hasa kutokana na doria zilizofanyika ikiwemo katika safu za milima ya Jaber ambayo inakaliwa na waasi” amesema Luteni Jenerali Ngondi.

Kwa Upande wake Mkuu wa Operesheni ya Jaber, Mara Lameck Kawiche ametoa mwito kwa wanajeshi wa Tanzania kuendeleza utayari  wao ili kuhakikisha  wanalinda heshima ya jeshi hilo kwa kufanya kazi kwa weledi ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea kama ilivyotokea nchini Kongo.


1 comment: