Sunday, 8 April 2018

Kemikali ya sumu yaua watu 100 Douma Syria


Rais wa Syria, Bashar al- Assaad

WAFANYAKAZI wa uokoaji pamoja na madaktari walioko katika eneo la Mashariki mwa Ghouta nchini Syria, wamethibitisha kuwa zaidi ya watu 90 wamefariki dunia katika shambulio baya la Kemikali.
Serikali ya Rais Bashar Al- Asaad wa Syria imekanusha kutumia kemikali hiyo ya sumu dhidi ya raia.
Idara ya kimataifa ya usalama nchini Marekani, inasema, inafuatilia kwa karibu mno taarifa zinazohuzunisha za matumizi ya silaha za kemikali wilayani Ghouta Mashariki.
Taarifa hiyo inasema kwamba, maofisa wakuu wanaamini zaidi ya watu 40 waliuawa, katika shambulio hilo, lakini ikaongeza kuwa, idadi kamili ya waliouawa, inaweza kuwa juu zaidi. Utawala wa Syria umekanusha kutekelezaji wa shambulio kama hilo.
Kundi la White Helmets, ambalo ni la utoaji msaada wa kujitolea, limechapisha picha za maiti nyingi kwenye mtandao wake wa kijamii, zikiwa ndani ya chumba kimoja kwenye ghorofa ya chini ya jumba moja, zikiwemo picha za wanawake na watoto waliofariki.
Picha hizo bado hazijathibitishwa. Awali, ilisemekana kuwa, watu 150 waliuawa, huku idadi hiyo ikitazamiwa kuongezeka.
Undani wa vita hivyo
Shambulio linaloshukiwa kuwa la kigaidi, lililolenga mji wa Douma, eneo linaloshikiliwa na waasi Mashariki mwa mji wa Ghouta, limetokea baada ya majuma kadhaa ya milipuko ya mabomu kutoka angani, iliyotekelezwa na wanajeshi wa Syria.
Raia wapatao laki moja, inasemekana wamekwama huko, kwa pamoja na wapiganaji waasi.
Runinga ya taiafa la Syria, inalilaumu kundi kuu la Waasi la Jaish al-Islam, kwa kutia chumvi kutokea kwa shambulio hilo, katika jaribio lililoshindwa ya kuzuia juhudi za Jeshi la Syria kuendelea mbele kuwakabili.
Kumekuwa na mashambulio kadhaa ya kemikali ambayo yametokea nchini Syria, katika mapigano hayo makali yaliyodumu kipindi cha miaka 7 iliyopita.

No comments:

Post a Comment