Saturday, 28 April 2018

Kim Jong Un akubali kuangamiza silaha za kinyuklia rasi ya Korea


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un (kushoto) akipeana mikono na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in.

VYOMBO vya habari vya Korea Kaskazini vimekuwa vikisifia mkutano wa jana uliokuwa wa kihistoria kwa namna nyingi ambapo miongoni mwa matukio ambayo kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un walikubaliana kufanya kazi pamoja na rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in, katika kile walichosema ni kuhakikisha hamna silaha za kinyuklia katika rasi nzima ya Korea.
Runinga ya serikali imemlimbikizia sifa na kumpa hongera Kim Jong-un kwa kufanikisha hayo wakisema ni kutokana na upendo wake kwa raia wake na kutaka pia nchi hiyo iweze kujitegemea.
Msimamo huo ni tofauti na jinsi vyombo vya habari vya Korea Kusini walivyouchambua mkutano huo.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema si rahisi kutabiri azma ya baadaye ya Kim Jong Un hasa katika suala la iwapo kweli atatupilia mbali miradi yake ya kinyuklia, wakihoji kuwa hakutoa hakikisho lolote linaloweza kuaminika.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema ataendelea kuishinikiza Korea Kaskazini kuachana na miradi yake ya kinyuklia licha ya mafanikio makubwa ya mkutano wa jana baina ya viongozi wa Korea Kusini na Kim Jong Un wa Korea Kaskazini.
Trump pia amesisitiza azma yake ya kukutana na kiongozi huyo wa Korea Kaskazini kwa matumaini kwamba ataweza kumshawishi asiendelee kujilimbikizia silaha hizo hatari.
Katika mkutano huo wa jana uliokuwa wa kihistoria kwa namna nyingi, Kim Jong un alikubaliana kufanya kazi pamoja na rais wa Korea Kusini, Moon Jae-in katika kuhakikisha hamna silaha za kinyuklia katika rasi nzima ya Korea.
Hata hivyo, wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema si rahisi kutabiri azma ya baadaye ya Kim Jong Un hasa kuhusu suala la iwapo kweli atatupilia mbali miradi yake ya kinyuklia.
Korea Kazkazini imewekewa vikwazo vya kiuchumi chungu mzima kutokana na kukataa kwake kusitisha miradi hiyo ya kinyuklia ambayo imekuwa ikiwatia wasiwasi jirani zake, Korea Kusini, Japan na washirika wao wa karibu Marekani wanaosema inawahatarishia usalama wao.
BBC

No comments:

Post a Comment