Tuesday, 24 April 2018

Kitukuu wa kiume wa Malkia Elizabeth azaliwa


KITUKUU wa sita wa Malkia Elizabeth amezaliwa jana saa 7 mchana kwa saa za Afrika Mashariki katika hospitali ya St.Mary iliyopo Lindo Wing huko mjini London, Uingereza.
Kuzaliwa kwa mtoto huyo wa tatu wa mwana wa Mfalme William na mke wake Catherine kumekuongeza furaha katika familia hiyo. Taarifa zinasema mama na mtoto huyo wa kiume wanaendelea vizuri.
Familia zote wamepata taarifa ya ujio wa mtoto huyo na wana furaha kwa habari hizo njema. Hadi sasa jina la mtoto mpya bado alijatangazwa.
Taarifa kutoka makazi ya malkia zinasema William alikuwepo wakati mtoto huyo akizaliwa na majina anayoyapenda kwenye vitabu ni pamoja na Arthur, Albert, Frederick, James na Philip.
Waziri mkuu wa nchi hiyo,Theresia May amewatumia salamu za pongezi, anawatakiwa furaha na maisha mema yajayo.

No comments:

Post a Comment