Tuesday, 17 April 2018

Kolimba afanya mazungumzo na Spika wa EALANaibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Susan Kolimba (kushoto), akiagana na mgeni wake Spika wa Bunge la EALA, Martin Ngoga baada ya mazungumzo yao ofisini kwake mjini Dodoma.

Mary Meshack, Dodoma


NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Susan Kolimba amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA) Martin Ngoga katika ofisi za wzara hiyo mjini Dodoma.

Katika mazungumzo yao,  Dk. Kolimba amemwahidi Spika Ngoga kuwa wizara na Serikali kwa ujumla itatoa ushirikiano wa hali ya juu kwa Bunge hilo katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwa na lengo la kuboresha ushirikiano baina ya nchi wanachama wa EALA.

Kwa upande wake Spika wa EALA amesema kwa sasa wamejipanga kuhakikisha wanadumisha ushirikiano na mabunge ya nchi wanachama na kutoa mrejesho kwa nchi wanachama kuhusu masuala mbalimbali ya yanayojili katika Bunge hilo.

Spika Ngoga yupo mkoani Dodoma ambapo Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki linaendelea na vikao vyake mjini humo ambavyo vimeanza April 9 na vinatarajiwa kumalizika April 28, mwaka huu (2018).

No comments:

Post a Comment