Sunday, 29 April 2018

Korea Kaskazini kufunga eneo la majaribio ya nyuklia


Kombora la masafa marefu la nyuklia
KOREA Kusini imesema Korea Kaskazini imeahidi mwezi ujao kufunga eneo lake la kufanyia majaribio ya nyuklia na itaalika wataalamu wa kimataifa na wanahabari kushuhudia kufungwa eneo hilo.
Ofisi wa ya rais nchini Korea Kusini imesema pia Korea Kaskazini imekubali kubadilisha saa zake kuwa sawa na za Korea Kusini, ikiwa ni ishara nzuri kwa kuwa kwa sasa saa ya Korea Kaskazini iko nusu saa nyuma ya ile ya Korea Kusini.
Korea Kusini inasema hatua hizo zinakuja baada ya mkutano wa kihistoria wa siku ya Ijumaa kati ya viongozi wa nchi hizo mbili. Pyongyang awali ilikuwa imetangaza kuwa eneo hilo la kufanyia majaribio lingefungwa.
Iliripotiwa kukana madai ya wanasayansi wa China kuwa eneo hilo lilikuwa limeharibiwa vibaya na halingeweza kutumiwa tena.
Siku ya Ijumaa, kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in walikutana kufanya kazi wakiwa pamoja kuondoa zana za nyuklia rasi ya Korea,
Mkutano huo ulfanyika miezi michache baada ya matamshi ya kivita kutoka Korea Kaskazini.
BBC

No comments:

Post a Comment