Sunday, 22 April 2018

Korea Kaskazini yadai kusitisha kwa muda majaribio ya silaha za kinyuklia


Kim Jong-Un

KIONGOZI wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un, ametangaza kusitishwa kwa muda shughuli zake za kufanya majaribio ya silaha zake za kinyuklia.
Kim amedai kwamba hamna haja ya kufanya tena majaribio kwa sababu nchi yake tayari imefanikiwa katika malengo yao ya kuwa wamiliki wa zana za kinyuklia
Tangazo hilo linajiria wakati kuna harakati za kujaribu kufanikisha maandalizi ya mikutano inayotarajiwa kufanyika baina ya kiongozi huyo wa Korea Kaskazini na rais wa Marekani, Donald Trump.

No comments:

Post a Comment