Friday, 13 April 2018

Kula parachichi unapojisikia uchovu wa mwilini


Parachini lenye ganda la kijani

PARACHICHI ambalo pia unaweza kuliita embe mafuta, na kwa lugha ya Kiingereza avocado, ni tunda lenye kokwa kubwa ndani na nyama ya kijani inayofunikwa na ganda lenye rangi ya kijani au nyeusi.
Asili ya tunda hili lenye radha iliyopoa ni Amerika ya Kati huku Wahispania wakitajwa kulipeleka katika maeneo mbalimbali duniani.
Mparachichi (mti wa parachichi) ndiyo unazaa tunda hili lenye utajiri wa vitamini ikiwemo A, B na C.
Pamoja na faida nyingine nyama ya parachichi inasaidia kuutia mwili asidi yuriki ambayo inasaidia kupambana na maradhi ya baridi yabisi, magonjwa ya ini, magonjwa ya ngozi, maradhi ya tumbo na gauti.
Licha ya kusaidia maradhi hayo, ukitumia juisi ya parachichi au kula tunda lenyewe, unapata nguvu ya mwili na ubongo, linasaidia kujenga neva za fahamu, kujenga mifupa, kuipa nguvu na kusaidia uoni kuwa mzuri.

Parachichi lenye ganda rangi ya zambarau
Majani ya parachichi yakichemshwa na kunywewa kama chai, yanasaidia kuondoa matatizo ya mwili kama uchovu, udhaifu, mwili kuwa ovyo, kuumwa kichwa, koo, tumbo, mapafu na uvimbe.
Pia ukitafuna majani ya parachichi yanasaidia tatizo la vidonda mdomoni (fizi), huimarisha meno na kuondoa maumivu.
Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.
Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com ili kupata ushauri au virutubisho vyetu vinavyopatikana kwa bei nafuu.

No comments:

Post a Comment