Saturday, 28 April 2018

Limeni chakula kwa wingi serikali haina mpango wa kugawa chakula cha msaada - Magufuli


Rais Dk. John Magufuli

Peter Simon

RAIS Dk. John Magufuli amewataka wananchi kufanya kazi hasa katika kilimo kwani serikali haina mpango wa kugawa chakula cha bure mwaka huu.

Rais Magufuli amesema hayo jana April 27, 2018 wakati akifungua barabara ya lami kutoka Dodoma hadi Babati, Manyara yenye urefu wa kilometa 251 ambayo imegharimu sh. bilioni 378. 

"Siwezi kuhangaika kutafuta fedha za kujenga barabara, kununua ndege, viwanja, halafu bado nitafute na fedha za kuwanunulia chakula cha bure. Nasema, hakuna chakula cha bure, ambaye hatalima, atakufa njaa.

"Mvua imeenyeesha miezi yote halafu ije itokee mwezi wa ngapi mseme tunaomba chakula  kuna njaa tutakufa nitasema tu kufa. Nawaambia Watanzania wote kuanzia Kongwa mpaka Chato hakuna chakula kitakachogawiwa mwaka huu," amesisitiza.

Hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini imeimarika na kufikia tani milioni 15.9 kwa msimu wa kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 sawa na kuwa na ziada ya tani milioni 2.6.

No comments:

Post a Comment