Wednesday, 11 April 2018

Lissu kufanyiwa oparesheni mara ya 20


Tundu Lissu 


Peter Simon

MBUNGE wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine leo.

Tundu Lissu yupo katika matibabu nchini Ubelgiji mara baada ya kushumbaliwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba mwaka jana, mjini Dodoma.

“Kama nilivyowataarifu siku za nyuma, mguu wa kulia bado una shida kutokana na risasi nyingi nilizopigwa na ‘watu wasiojulikana, operesheni ya leo ni sehemu ya tiba ya mguu huo.

Napenda wote mfahamu kwamba niko kwenye mikono salama ya kitabibu. Mungu wetu amekuwa mwema sana kwangu tangu  Septemba 7 ya mwaka jana,” amesema Tundu Lissu.

Kabla ya kupelekwa Ubelgiji kwa ajili ya matibu zaidi, Lissu alikuwa akipokea matibabu Nairobi nchini Kenya ambapo Decemba 26 aliweza kusimama kwa mara ya kwanza tangu aliposhambuliwa. January 07, 2018 ndipo aliwasili Ubelgiji.

No comments:

Post a Comment