Sunday, 22 April 2018

Madai dhidi ya wizi wa almasi Mugabe atakiwa kutoa ushahidi


Robert Mugabe 
BUNGE  la Zimbabwe limemtaka Rais wa zamani wa taifa hilo, Robert Mugabe kutoa ushahidi wa madai aliyotoa kuhusu wizi wa almasi.
Mugabe alizishutumu kampuni za kigeni za kuchimba madini kwa ''kuiba'' na ''kusafirisha'' katika mahojiano na runinga ya taifa 2016.
''Kampuni hizo zimetuibia utajiri wetu'' , alisema. Akiongezea kuwa wizara ya fedha ilipokea dola za Marekani bilioni 15.
Haijulikani iwapo Mugabe mwenye umri wa miaka 94 atakubali kufika mbele ya kamati hiyo ya bunge.
Alilazimishwa kujiuzulu mwezi Desemba mwaka jana baada ya mapinduzi ya kijeshi na bado anahudumiwa na serikali kama rais wa zamani.

No comments:

Post a Comment