Dk. John Magufuli (kushoto) na Jumanne Ngoma
Mwandishi Wetu, Manyara
RAIS Dk. John Magufuli amesema Serikali inampa sh. milioni 100 Jumanne Ngoma aliyegundua madini ya Tanzanite mkoani Manyara.
Rais Magufuli ameyasema hayo jana Aprili 6 wakati wa uzinduzi wa
ukuta wa mgodi wa Tanzanite, Mirerani mkoani humo.
"Watu hawa hawatambuliwi, tazama mzee huyu, ndiye
aliyegundua madini haya, leo tusingekuwapo hapa kama asingekuwa huyu mzee.
Tazama sasa amepooza mguu wake,” amesema.
Amebainisha kuwa mzee huyo hakutakiwa kuketi katika viti vya
nyuma wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa ukuta wa mgodi huo.
Baada ya Rais Magufuli kumuulizia Mzee Ngoma, aliletwa
kuketi mbele, akiwa ameshikiliwa kutokana na miguu yake kupooza.
Rais Magufuli amesema fedha hizo zimsaidie katika matibabu yake
na katika mahitaji yake mengine.
No comments:
Post a Comment